Raia wa Uingereza kupimwa Covid-19 mara mbili kwa wiki

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amesema hivi karibuni raia wa taifa hilo watakuwa na fursa ya kupimwa ugonjwa wa Covid-19 mara mbili kwa wiki, huku nchi hiyo ikitafakari maisha baada ya janga la Corona.

Johnson alisema siku ya Jumatatu kwamba mpango huo utazima msururu wa visa vya maambukizi na kusaidia kutambua ishara zozote za ugonjwa huo, ambazo zinaaminika kuchukua kisa kimoja kati ya vitatu vya maambukizi mapya. 

Mpango huo wa kuwapima halaiki nchini humo ambao unatarajiwa kuanza siku ya ijumaa, utakuwa ukitumia vifaa ambavyo vinaweza kutoa matokeo kwa muda wa dakika 30 na watu hawatakuwa wakilipishwa chochote.

Juma lijalo Uingereza inatarajiwa kulegeza masharti zaidi, hali ambayo inatokana na kutolewa kwa haraka kwa chanjo dhidi ya virusi hivyo.

Zaidi ya watu milioni tano wamechanjwa kwa kutumia chanjo za Oxford-AstraZeneca na Pfizer-BioNTech.

Uingereza ilikuwa na vifo elfu 126 vilivyosababishwa na ugonjwa huo na kuorodheshwa ya tano duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *