Raia nchini Uingereza waanza kupokea chanjo dhidi ya Covid-19

Ajuza wa miaka 90 kutoka Ireland kaskazini ndiye mtu wa kwanza duniani kupokea chanjo ya Pfizer/BioNTech dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Margaret Keenan kutoka Enniskillen alisema alifurahia sana kupokea chanjo hiyo huku watu nchini Uingereza wakitarajiwa kuanza kupokea chanjo hiyo ya ugonjwa wa Corona.

Takriban taasisi 70 za kimatibabu kote nchini humo zinajitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo ya kampuni ya dawa ya  Pfizer kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 pamoja na baadhi ya maafisa wa kimatibabu.

Mpango huo unalenga kuwalinda wakongwe dhidi ya maambukizi hayo.

Dkt Hari Shukla mwenye umri wa miaka  87 aliyepia babu wa wajuku 11 alisema ana furaha kutekeleza wajibu wake kwa kuchanjwa.

Uingereza itakuwa taifa la kwanza duniani kuanza kutumia chanjo hiyo ya kampuni ya Pfizer baada ya matumizi yake kuidhinishwa wiki jana.

Watakao toa chanjo hiyo,watakuwa wa kwanza kuchanjwa huko Scotland, huku wahudumu wa afya watakuwa wa kwanza kuchanjwa huko Wales na Ireland kaskazini.

Waziri mkuu Boris Johnson alisema kuzinduliwa kwa shughuli hiyo ya chanjo,ni hatua kubwa kwenye vita dhidi ya Corona nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *