Polisi wanamsaka mtu mmoja aliyemuua rafikiye kwa kumteketeza

Maafisa wa idara ya upelelezi wa Jinai (DCI), wanamtafuta mtu mmoja aliyeaminika kumuua rafikiye wa zamani katika mtaa wa Njiru jijini Nairobi siku ya Alhamisi kwa kumteketeza akiwa nyumbani mwake kabla ya kutoroka.

Ripoti ya wafanyikazi wawili wa nyumba ya marehemu inasimulia jinsi mwajiri wao, baada ya kumpokea mgeni mwendo wa saa mbili asubuhi aliwapa nafasi ya kwenda mapumzikoni ili wawe na muda wa kujadili mambo yao.

Maafisa wa upepelezi wanasema ilipotimu alasiri, nyumba hiyo ilionekana ikiteketea, na hakuna chochote kilichookolewa baada ya moto huo kuzimwa.

Mwili wake ulioteketea, ambapo mikono iliyoonekana kufungwa kabla ya nyumba hiyo kuteketezwa ilipatikana mahala hapo.

Maafisa wa (DCI) kutoka eneo la Kayole wanashirikiana na wenzao wa kitengo cha utafiti kuhusu uhalifu na ujasusi katika kumsaka mtu huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *