Polisi wakabiliana na waandamanaji wanaopinga sheria mpya Ufaransa

Waandamanaji kadhaa wamepambana na polisi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, dhidi ya mswada wa sheria uliozua utata.

Polisi walifyatua vitoza machozi hewani ili kuwatawanya waandamanaji wanaodaiwa kutumia fursa hiyo kupora maduka na kuvunja vioo vya madirisha ya maduka, na kuteketeza magari kadhaa.

Takriban mikutano 100 ya maandamano imepangwa kufanywa kote nchini humo, kupinga mswada huo wa sheria, ambao utaharamisha upigaji picha wa polisi wanapotekeleza majukumu yao.

Wanaopinga mswada huo wa sheria ambao wanasema utakandamiza uhuru wa vyombo vya habari, hasa vinapofwatilia habari kuhusu ukatili wa polisi.

Taifa hilo limeshuhudia maandamano ya kupinga sheria hiyo, na yalifikia upeo pale maafisa watatu wa polisi walipoonekana kwenye picha za video mtandaoni, wakimtusi na kumpiga mwanamuziki mmoja mweusi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macnon, alitoa hakikisho kuwa sheria hiyo itafanyiwa marekebisho.

Hata hivyo hakikisho hilo halijawaridhisha waandamanaji hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *