Pogba kusalia Old Traford hadi mwaka 2022

Kiungo wa Manchester United Pual Pogba atasalia katika timu ya Manchester United hadi mwaka 2022 baada ya kuongeza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake.

kandarasi ya awali ya Mfansa huyo aliye na umri wa miaka 27 ilitazamiwa kukamilika mwishoni mwa msimu huu.

Hii ina maana kuwa Real Madrid ambao wamekuwa wakisaka sahihi yake itabidi wasubiri hadi mwaka 2022.

Pogba alijiunga na Man United mwaka 2016 kwa pauni milioni 89 kutoka Juventus lakini alicheza meche 22 pekee msimu uliopita baada ya kutatizwa na msururu wa majeraha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *