Pickford aponea kuadhibiwa kwa kumvunja Van Dijk

Kipa wa Everton Jordan Pickford aponea kuadhibiwa kwa kumvunja Van Dijk

Mlinda lango wa  Everton Jordan Pickford ameepuka kuadhibiwa na chama cha soka nchini Uingereza kwa kosa la kumvunja beki tegemeo wa Liverpool Virgil van Dijk katika mechi ya derby ya  Merseyside iliyoishia sare ya mabao 2-2 Jumamosi iliyopita ugani Goodison Park.

Mwamuzi mkuu wa pambano hilo  Michael Oliver alishuhudia kisa hicho na ilikuwa imekisiwa kuwa Pickford ambaye ni kipa nambari moja wa Uingereza akishutumiwa vikali kwa kosa hilo.

Hili ni pigo kubwa kwa Liverpool kumpoteza Van Dijk  ambaye amekuwa beki kisiki katika timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *