Pesa za London marathon mwaka 2020 zapunguzwa

Waaandalizi wa mashindano ya London marathon wametangaza kupunguza kiwango cha pesa zitakazotuzwa washindi wa mbio za mwaka huu  kutokana na makali ya  Janga la Covid 19.

Washindi wa mbio za wanariadha wa kulipwa katika mashindano ya London marathon wamekuwa wakilipwa dola 55,000,kiwango ambacho huenda kikapunguzwa kwa takriban nusu huku bajeti ya zawadi ambayo imekuwa zaidi ya dola 300,000 pia ikikatwa kwa takriban nusu .

Waandalizi wa mbio  hizo wametangaza kuwa wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya janga la ugonjwa wa Covid 19 lililoathiri ulimwengu kuanzia mapema mwaka huu  na kusababisha shughuli za michezo kusitishwa.

Watayarishi wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za London marathon wamepunguza kwa nusu kiwango cha pesa zitakazoshindaliwa tarehe 4 mwezi ujao katika makala ya mwaka 2020 ya London marathon kutokana na uhaba wa pesa uliosababishwa na Covid 19.

Wanariadha wa Uingereza bora kwenye  mbio hizo pia wametengewa kiwango tofauti cha zawadi ya pesa kwa mara ya kwanza.

Mbio za mwaka huu kwa mara ya kwanza zitaandaliwa mwezi Oktoba baada ya kuahirishwa kutoka mwezi April .

Washikilizi wa rekodi za dunia Brigid Kosgei na Eliud Kipchoge wametoa ithibati ya  kutetea mataji yao ya mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *