Categories
Michezo

Pamzo ateuliwa kocha msaidizi wa Gor Mahia

Sammy ‘Pamzo Omollo’ ameteuliwa kuwa naibu kocha wa mabingwa wa Kenya Gor Mahia .

Omollo, ambaye alikuwa beki wa zamani wa Kogalo anatarajiwa kusafiri na timu hiyo kwa mechi ya marudio kufuzu kwa hatua ya makundi Jumapili dhidi ya NAPSA Stars ya Zambia.

Omollo anatwaa mikoba hiyo ya naibu kocha wa Kogalo  kusaidiana na kocha mkuu  Mreno Carlos Manuel Vaz Pinto na ndiye naibu kocha wa kwanza tangu kuondoka kwa Patrick Odhiambo  aliyehamia Kakamega Homeboyz.

Kocha huyo hajakuwa na kibarua tangu afurushwe Posta Rangers akiwa kocha mkuu kutokana na matokeo mabovu,na ni mara yake ya pili kurejea Gor baada ya kuwa usukani katika mechi za ligi ya mabingwa msimu huu .

Gor Mahia walioshindwa bao 1-0 katika mkumbo wa kwanza wiki jana watawania ushindi wa magoli 2-0 Jumapili ili kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *