Osaka bingwa wa Us Open 2020

Naomi Osaka ndiye mshindi wa taji ya Us Open, baada ya kumshinda  Vitoria Azarenka  wa Belarus seti 2-1 mapema leo .

Osaka aliye na umri wa miaka 22 kutoka Japan  ameshinda taji yake ya tatu ya Grand Slam,na licha ya kupoteza seti ya kwanza pointi 1-6,alirejea na kutwaa seti 2 zilizofuatia 6-3 na 6-3 .

Azarenka aliye na miaka 31 alikuwa akiwania taji yake ya kwanza kuu tangu mwaka 2013  .

“nimefurahi sana kucheza nawe,kwani umekuwa kielelezo kwangu,nimekuwa nikikutazama ukicheza tangu nikiwa mdogo”Osaka alimwelezea Azaarenka baada ya mechi.

Naomi Osaka akicheza fainali

Osaka  ambaye amekuwa akishikilia nafasi ya 4 ulimwenguni sasa ndiye mchezaji bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *