Orodha ya mwisho ya waaniaji viti vya Fkf yatangazwa

Bodi inayosimamia uchaguzi wa Fkf, imekamillisha kupokea na kusikiza malalamishi yanayohusu zoezi hilo na kuchapisha orodha ya mwisho ya walioidhinishwa kuwania nyadhifa mbal mbali.

Viti vyote vya ueyekiti wa kaunti 47 vina wapinzani huku viti vya  4 vya Nec kati ya vyote 10 vikiwa waaniaji walioteuliwa bila kupingwa.

Kiti cha Nec Nairobi kimewavutia  Tom Alila,Isaac Macharia mwenyekiti anayeondoka wa fkf Nairobi East Ouma Majua.

Waaniaji watano wameidhinishwa kuwania Urais wa Fkf akiwemo Lodvick Aduda ambaye ni Ceo wa Gor Mahia,aliyekuwa mwenyekiti wa Afc Leopards Dan mule,mwanahabari Boniface Osano na Herbert Mwachiro wanaompinga rais wa  sasa Nick Mwendwa anayetatufa muhula wa pili.

Uchaguzi huo ambao unaandaliwa kwa mara ya tatu baada ya kufutiliwa mbali mara mbili na mahakama ya michezo nchini,umezua utata tena huku baadhi ya waaniaji wa Urais akiwemo Sam Nyamweya,Sammy Sholei,Nicholas Musonye na Twaha Mubarak wakijiondoa kwa madai kuhisi ukosefu wa uwazi katika zoezi hilo na kukosa imani na bodi ya uchaguzi.

Orodha kamili ya waliodhinishwa kuwania viti mbalimbali ni kama ifuatavyo:-

http://County: https://bit.ly/3il7qLp—majina ya wagombeaji viti vya kaunti

NEC: https://bit.ly/3bMncfy—–majina ya wagombeaji  viti vya NEC

Presidential: https://bit.ly/32i1v44——Majina ya wagombeaji wa Urais

Bodi hiyo inayoongozwa na mwenyekiti Kentice Tikolo itaandaa uchaguzi wa kaunti tarehe 19 mwezi huu ,ukifuatiwa na ule wa Kitaifa Oktoba 19.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *