Ongezeko la visa vya ajali za pikipiki katika eneo la pwani lahofisha

Mrakibu wa eneo la pwani, John Elungata amefadhaishwa na ongezeko la vifo vinavyosababishwa na ajali za pikipiki.

Elungata amesema maafisa wa polisi pamoja na halmashauri ya usalama na uchukuzi wanafuatilia hali hiyo na wameahidi kuanzisha msako mkali dhidi ya wale wanaokiuka sheria za barabarani.

Akiongea wakati wa mkutano wa kamati ya utekelezaji mipango Katika eneo hilo mjini Mombasa,  Elungata aliagiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya waendeshaji pikipiki, tuk tuk na magari mengine ambao hawazingatii kanuni zilizowekwa.

“Wengi wa waendeshaji pikipiki na tuktuk, hujifunza wenyewe kisha wanapata leseni bila kupata mafunzo rasmi na hivyo kuhatarisha maisha ya wateja wao,” alisema elung’ata

Alihimiza halmashauri ya usalama na uchukuzi NTSA, kurejelea mafunzo kuhusu usalama na kushtakiwa kwa waendeshaji pikipiki wasiozingatia sheria ili kupunguza idadi ya vifo.

Alitaja barabara ya kutoka Kilif kuelekea Malindi pamoja na zile za kaunti za Tana River na Mombasa kama baadhi ya zile ambako ajali za pikikpiki zimekithiri.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *