Categories
Michezo

Omollo acheza dakika 90 katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu Uturuki

Kiungo wa Kenya Johanna Omollo alicheza dakika zote 90  katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ,huku timu yake ya Ezrum BB ikisajili ushindi wa  mabao 2-1 ugenini  dhidi ya  Kasimpsa  Jumatatu usiku .

Omollo aliye na umri wa miaka 31  alisajiliwa na klabu hiyo wiki jana kutoka Cercle Brugge ya Ubelgiji na ndiye Mkenya wa kwanza kupiga soka ya kulipwa nchini Uturuki.

Johanna Omolo (KATIKATI) akiwa mazoezini kabla ya mechi Jumanne

Ushindi huo unafufua matumaini ya Ezrumm kusalia ligini wakiwa wamezoa pointi 16 kutokana na mechi 19.

Besiktas na Fernabache zinaongoza jedwali la ligi hiyo kwa alama 38 kila moja pointi 4 zaidi ya Gaziantep iliyo ya tatu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *