Omollo acheza dakika 90 katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu Uturuki
Kiungo wa Kenya Johanna Omollo alicheza dakika zote 90 katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ,huku timu yake ya Ezrum BB ikisajili ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Kasimpsa Jumatatu usiku .
Omollo aliye na umri wa miaka 31 alisajiliwa na klabu hiyo wiki jana kutoka Cercle Brugge ya Ubelgiji na ndiye Mkenya wa kwanza kupiga soka ya kulipwa nchini Uturuki.

Ushindi huo unafufua matumaini ya Ezrumm kusalia ligini wakiwa wamezoa pointi 16 kutokana na mechi 19.
Besiktas na Fernabache zinaongoza jedwali la ligi hiyo kwa alama 38 kila moja pointi 4 zaidi ya Gaziantep iliyo ya tatu.