Olunga azidisha uchu wa kufunga mabao nchini Japan

Mshambulizi matata wa Harambee stars Michael Ogada Olunga alipachika kimiani bao moja ,huku timu yake ya Kashiwa Reysol ikiambulia kichapo cha mabao 3-2 ugenini dhidi ya Shonan Belmare katika pambano la ligi kuu mapema Jumapili.

Olunga alifunga bao la kwanza katika dakika ya 22 kufuatia pasi ya Cristiano,likiwa bao la kusawazisha baada ya Takuyo Okamoto kuwaweka wenyeji kifua mbele mwanzoni mwa mechi.

kufuatia kipigo cha Jumapili Kashiwa ni ya nane ligini kwa pointi 37 kufuatia mechi 23,wakati Kawasaki Frontale wakiongoza kwa alama 65 kutokana na mechi 24.

Olunga anaonekana kutoroka na kiatu cha dhahabu au tuzo ya mfungaji bora katika ligi hiyo ya Japan akiwa amecheka na nyavu mara 22 huku wapizani wake wa karibu wakiwa na mabao 12 kila mmoja.

Mshambulizi huyo aliyezichezea Thika united,Tusker fc na Gor Mahia alilishwa kadi ya njano mwishoni mwa mchuano huo kwa utovu wa nidhamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *