Olunga arejea kutoka Karantini kwa kishindo na kufunga bao

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga amepachika bao moja huku timu yake  ya  Kashiwa Reysol ikiambulia kichapo cha mabao 1-2 nyumbani  mapema Jumamosi katika mechi ya ligi kuu ya Japan.

Kashiwa walikuwa chini mabao 2-0 hadi dakika ya 87 wakati Olunga alipokomboa bao hilo moja lakini tayari maji yalikuwa yamezidi unga.

Kwa jumla Olunga angali kuongoza chati ya ufungaji mabao kwenye ligi kuu ya Japan kwa ambao 24 ,magoli 8 zaidi ya Everaldo wa Kashima aliye wa pili .

Kipigo cha Kashiwa kinawaacha katika nafasi ya 10 kwa alama 41 kutokana na mechi  27.

Tiimu ya Olunga itawazuru Kashima Antlers Novemba 25 kwa pambano la raundi ya 28 ya ligi kuu.

Kashiwa ambao walikuwa wanacheza mchuano wa kwanza wa ligi tangu  Oktoba 31 wakati wachezaji wote walilazimishwa kuingia Karantini  baada ya wachezaji watatu kupatikana na homa ya Korona.

Hatua hiyo ilichangia kuzuiwa kwa Olunga kusafiri kuja Kenya kushiriki mechi ya kufuzu kwa kombe la AFCON dhidi ya Comoros.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *