Olunga apiga mechi ya kwanza Al Duhail

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alicheza dakika 67 za mechi yake ya kwanza na timu mpya ya Al Duhail katika ligi kuu ya soka nchini Qatar Jumanne usiku,huku timu yake ikiambulia kichapo cha mabao 3-1 ugenini dhidi ya viongozi wa ligi Al Saad.

Olunga aliye na umri wa miaka 26 alianza mchuano huo siku moja baada ya kusaini mkataba wa donge nono na wa Takriban shilingi milioni 930 za Kenya akitokea Kashiwa Reysol  ya Japan aliyoichezea kwa miaka miwili .

Mshambuluzi huyo ambaye zamani alikuwa na timu za Mathare United,Gor Mahia na Tusker Fc atakuwa akilipwa mshahara wa shilingi milioni 16 kwa mwezi katika mkataba huo mpya na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu zamani wakijulikana kama Lakhwiya .

Ushinde huo unaicha Al Duhail alama 8 nyuma ya viongozi Alasaad baada ya mechi 14 za ligi kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *