Olunga apiga dakika 46 huku ndoto yake ya kucheza na Bayern Munich ikizimwa na Al Ahly

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alicheza dakika 46 kabla ya kuondolewa uwanjani katika ushinde wa timu yake  ya Al Duhail Sc wa bao  1 na mabingwa wa Afrika Al Ahly katika kwota fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu  katika uwanja wa Education City Stadium mjini  Al Rayyan nchini Qatar Alhamisi usiku.

Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Olunga kucheza katika fainali hizo za kombe la dunia akiwakilisha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Qatar tangu ajiunge  nao mwezi uliopita kutoka kashiwa Reysol ya Japan.

Tobwe la Hussein El Shahat kunako dakika ya 30 liliotosha kuwapa Ahly maarufu Red Devils kutoka Misri ushindi huo ambao uliwafuzisha kwa nusu fainali watakapochuana na mabingwa wa ulaya Bayern Munich Februari 8 wakilenga kuwa timu ya pili ya Afrika kucheza fainali ya kombe hilo baada ya TP Mazembe ya Jamhuri ya demokrasia ya Congo.

Katika mechi nyingi ya robo fainali mabingwa wa Marekani Kaskazini  Tigres UNL ya Mexico waliibandua Ulsan Hyundai ya Korea Kusini mabao 2-1 na kufuzu kwa nusu fainali kuchuana na mabingwa wa Amerika Kusini  Palmeiras ya Brazil .

Al Duhail watarejea uwanjani dhidi ya mabingwa wa Asia Ulsan kuwania nafasi ya 5 na 6 tarehe 7 kabla ya fainali ya tarehe  11 mwezi huu.

Mashindano hayo hushirikisha  mabingwa wa kila bara na huandaliwa kila mwaka .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *