Olunga anusia tuzo ya mfungaji bora Japan

Michael Olunga  anakaribia kunyakua tuzo ya mfungaji bora kwenye ligi kuu ya soka nchini Japan  J league 1 baada  ya kufunga bao moja katika ushindi wa timu yake ya Kashiwa Reysol wa mabao 4-1 Jumatano adhuhuri  dhidi ya  Kashima Antlers  uwanjani Kashima Soccer .

Bao la Olunga lilikuwa lake la 25  msimu huu ,huku akiongoza chati ya ufungaji mabao  wakati timu yake ikisalia ya 10 kwa pointi 44 kutokana na michuano 28.

Kashiwa watakuwa ugenini kwa  Vegalta Sendai Disemba 1 pambano lililoahirishwa kutoka Novemba 3 kutoka na janga la covid 19 timuni.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *