Olunga ajiuanga Al Dhuhail Fc ya Qatar

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na Al Dhuhail Sports Club ya Qatar akitokea  Kashiwa Reysol ya Japan aliyoichezea kwa miaka miwili.

Olunga aliye na umri wa miaka 26  aliibuka mfungaji bora msimu jana katika ligi kuu ya Japan akipachika mabao 28 na pia kutawazwa mchezaji bora kwenye ligi hiyo ya J1 league.

Yamkini Olunga atakuwa akilipwa  mara mbili ya mshahara wa shilingi milioni 8 aliokuwa akilipwa kwa mwezi katika timu ya Kashiwa  huku mkataba huo ukigharimu takriban shilingi bilioni 1.

Hii ina maana kuwa Olunga ambaye zamani alikuwa na vilabu vya  Thika United,Tusker Fc na Gor Mahia kwa mkopo atakuwa akitia kibindoni shilingi milioni 16 za Kenya  kwa mwezi.

Al Dhuhail ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Qatar zamani wakifahamika  kama Al Lakwiya na kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwa pointi 27 kufuatia mechi 13 nyuma ya viongozi Al Saad walio na alama 35.

Olunga  anafuata mkondo wa wachezaji wengi nyota wanaoichezea Al Duhail wakiwemo nahodha wa zamani wa Moroko Mehdhi Benatia ,Dudu wa Brazil ,mshambulizi wa Tunisia Yousef Msakni na wa hivi punde kuichezea akiwa Mario Mandzukic kabla ya kutamatisha kandarasi yake .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *