Olunga aibuka mfungaji bora ligi kuu Japan kwa mabao 28

Michael Olunga Ogada ametawazwa mfungaji bora ligi kuu nchini Japan huku msimu wa ligi hiyo ukifikia tamati mapema Jumamosi akifunga jumla ya mabao 28 ,magoli 10 zaidi Everaldo wa Kashima Antlers .

Olunga alifunga bao lake la 28 katika mechi ya kufunga msimu wakati timu yake ya Kashiwa ilipopoteza mabao 3-2 nyumbani na mabingwa wa ligi Kawasaki Frontale.

Kwa Jumla mshambulizi huyo wa Harambee Stars amefunga bao moja zaidi ya  27 aliyofunga msimu uliopita akiisaidia Kashiwa kupandishwa ngazi hadi ligi kuu kutoka J League 2 .

Kilabu ya Kashiwa ilifunga jumla ya mabao 60 ,na kufungwa  46.

Frontale wametwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa pointi 83 wakifuatwa na Gamba Osaka kwa alama 65  wakati Nagoya Grampus ikiibuka ya 3 kwa pointi 63 .

Kashiwa Reysol imemaliza katika nafasi ya 7 kwa alama 52 kutokana na mechi 34 ,wakishinda 15 kutoka sare 7 na kushindwa mechi 12 .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *