Categories
Habari

ODM yaunga mkono kubanduliwa kwa Gavana wa Migori Okoth Obado

Muungano wa vijana wa chama cha ODM ulikutana jana katika hoteli moja ya Machakos ambapo waliazimia kwamba wanaunga mkono kubanduliwa kwa Gavana wa Kaunti ya Migori Okoth Obado huku wakilihimiza Bunge la Kaunti hiyo liharakishe shughuli hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha ODM, Edwin Sifuna, alipongeza uamuzi huo, akisema kesi ya Obado haifanani na kesi zinazowakabili magavana wengine wa ODM ambao wameshtakiwa kwa ufisadi kwa sababu kwenye kesi ya Obado, mahakama imemzuia kuingia ofisini mwake.

Walikubaliana kuunga mkono mpango wa BBI kwa sababu ulianzishwa na kiongozi wa chama chao, Raila Odinga na rais kwa lengo la kuiunganisha nchi hii.

Pia waliazimia kuepuka kutumiwa kuzusha ghasia wakati wa kampeini huku wakiwaonya viongozi wanaotoa matamshi kiholela kwamba hawatatikiswa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *