Obiri kuwatumbuiza mashabiki Kip Keino Classic

Bingwa wa dunia Hellen Obiri atawaongoza wanariadha wengine kutoka humu nchini kudhihirisha ubabe wao atakapojitosa uwanjani jumamosi jioni kutimka mbio za mita 5000 katika mashindano ya Kip Keino Classic continental tour.

Obiri atafunga msimu katika uwanja wa taifa wa Nyayo baada ya kuweka muda wa kazi katika mashindano mawili kati ya mitatu ya Diamond league aliyoshiriki msimu huu uliopanza mwezi Agosti.

Mwanzo aliweka muda wa kasi katika mkondo wa Monaco katika mita 5000 na baaade mwezi uliopita akasajili muda wa kasi katika mkondo wa Doha Qatar.

Sasa Obiri anaahidi kuwapa mashabiki wa Kenya burudani atakapofyatuka mita 5000 jumamosi jioni katika mbio hizo ambazo ni za mwisho kwake mwaka huu.

Lakini kulingana na Obiri azma yake ya mwaka huu iliathiriwa pakubwa na ugonjwa wa Covid 19 ,na sasa atalenga taji ya Olimpiki mwaka ujao kabla ya kuhamia mbio za barabarani.

‘’Ni vyema na fahari kuu kukimbia nyumbani mbele ya mashabiki wa nyumbani na natarajia kufanya makuu ‘’akasema Obiri

Obiri ambaye hufanya mazoezi katika milima ya Ngong atakabiliana na wanariadha wa humu nchini katika mashindano ya Kip Keino Classic kama vila  Agnes  Ngetich,bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za nyika Agnes Jebet Tirop,Beatrice Chebet ,Sheilla Chepkurui dhidi ya Waethiopia Tigist Ketema,Sarah Chelangat kutoka Uganda  na Fantu Worku kutoka Ethiopia.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *