Obiri afungua msimu wa riadha Kenya kwa ushindi

Bingwa wa dunia katika mbio za nyika Hellen Obiri alianza msimu wa mwaka 2020/2021 kwa kishindo alipostahimili ukinzani mkali  na kutwaa ushindi wa mbio za kilomita10 katika msururu wa kwanza wa mbio za nyika nchini ulioandaliwa Jumamosi katika uwanja wa Machakos People’s Park.

Obiri akitimka uwanjani Machakos People’s Park

Obiri ambaye ni bingwa wa dunia katika mita 5000 alistahimili baridi na matope katika uwanja huo na kuwaacha wenzake huku akikata utepe kwa dakika 32 sekunde 29 nukta 2, akifuatwa na Caroline Nyaga wa Kenya Police kwa dakika 32 sekunde 46 nukta 8 ,huku Winfred Mutile kutoka Bahrain akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 32 sekunde 47 nukta 5.

Daniel Simyu kutoka Iten alishinda mbio za wanaume alipotimka kwa dakika 28 sekunde 27 nukta 7, akifuatiwa kwenye nafasi ya pili na Isaac Kibet kwa dakika 28 sekunde 54 nukta 6, huku Elvis Cheboi kutoka Elgeyo Marakwet akiambulia nafasi ya tatu kwa dakika 28 sekunde 54 nukta 9.

Obiri akielekea kumaliza mbio z akilomita 10 Jumamosi uwnajani Machakos people’s park

Kwenye matokeo ya kilomita 8 kwa wavulana chini ya umri wa miaka 20 ,Emmanuel Maru kutoka Iten aliongoza kwa dakika 22 sekunde 48 nukta 8 akifuatwa na Joseph Waweru wa Kajiado kwa dakika 23 sekunde 4 nukta 3 naye Victor Kipkurui wa Kericho akafunga ukurasa wa tatu bora kwa dakika 23 sekunde 8  nukta 4.

Felociana Jepkosgei wa Iten aliongoza kilomita 6 wasichana wasiozidi umri wa miaka 20  alipofyatuka kwa dakika 19 sekunde 21 nukta 6 ,akifuatwa na Grace Loibach kutoka Uasin Gishu kwa dakika 19 skunde  28 nukta 8, huku Edna Jepkemboi kutoka Nakuru akiridhika na nafasi ya tatu kwa dakika 20  sekunde 10 nukta 7.

Yafuatayo ni matokeo mseto ya Jumamosi

Kilomita 10 wanawake

Hellen Obiri (MAB) 32:29.2

Caroline Nyaga (Police) 32:46.8

Winfred Mutile (Individual) 32:47.5

Kilomita 10 wanaume

Daniel Simiu (Iten) 28:27.7

Isaac Kibet (Mount Elgon) 28:54.6

Elvis Cheboi (Elgeyo Marakwet) 28:54.9

kiliomita 8 wavulana chini ya umri wa miaka 20

Emmanuel Maru (Iten) 22:48.8

Joseph Waweru (Kajiado) 23:04.3

Victor Kipkirui (Kericho) 23:08.4

killomita 6 wasichana wasiozdi umri wa miaka  20

Felociana Jepkosgei (Iten) 19:21.6

Grace Loibach (Uasin Gishu) 19:28.8

Edna Chepkemboi (Nakuru) 201:10.7

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *