Noti 1000 nchini Argentina kuwa na picha ya Maradona

 

Seneta mmoja wa bunge la Argentina aliwasilisha mswaada bungeni siku ya Jumatatu kutaka picha ya Diego Maradona ichapishwe katika noti zote za viwango vya  1000 vya noti za nchini humo  maarufu kama Peso ,kama njia moja ya kumuenzi na kumkumbuka marehemu aliyefariki mwezi uliopita.

Kwa mjibu wa Seneta huyo anayejulikana kama Norma Durango , noti hiyo ya Peso 1000 itakuwa na picha ya marehemu Maradona upande mmoja huku upande wa pili ukiwa na picha ya bao lake maarufu la hand of God alilofunga kwa kutumia mkono katika robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Uingereza mwaka 1986 .

Maradona alifariki Novemba 25 mwaka huu alifunga mabao mawili maarufu katika fainali za kombe la dunia mwaka 1986 moja likiwa la hand of God kwenye robo fainali ya kombe la dunia lililoibandua Uingereza na  na jingine kwenye mechi ya  nusu fainali iliyowawezesha Argentina kuwashinda Ubelgiji mabao  2-0 na baadae kunyakua kombe la dunia  mwaka huo  kwa kuishinda Ujermani magharibi mabao 3-2 akiwa nahodha ingawa hakufunga bao .

Kumekuwa na ubishi kuhusu matumizi ya bao la hand of God katika noti  na stakabadhi za serikali  nchini humo ,wengi wakidai kuwa picha hiyo ikitumika itakuwa sawa na kuhalalisha haramu.

Mswaada wa seneta huyo wa mkoa wa La Pampa utasikizwa na bunge la Senate mapema mwaka ujao

Noti moja ya peso 1000 ni sawa na shilingi 1300 za Kenya .

Noti za sasa za 1000 nchini Argentina zina picha ya ndege .

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *