Categories
Habari

Ni mwanafunzi mmoja aliyeambukizwa covid-19 tangu kufunguliwa kwa shule

Wizara ya afya imesema ni kisa kimoja pekee cha maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kimeripotiwa miongoni mwa wanafunzi tangu shule zilipofunguliwa  majuma matatu yaliopita.

Hiyo kulingana na Waziri wa afya Mutahi Kagwe ni ishara kwamba nchi hii imo kwenye mwelekeo unaofaa.

Waziri hata hivyo alisema nchi hii imethibitishwa visa vingine 136 vya maambukizi ya ugonjwa huo kutoka kwa sampuli 3,787 zilizopimwa.

Visa hivyo vipya vimeongeza idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa hapa nchini hadi  99,444.

Alisema kiwango cha maambukizi hapa nchini kingali chini ya asilimia tano .Kati ya visa hivyo vipya,117 ni Wakenya huku 19  wakiwa raia kigeni.

85 ni wanaume ilhali 51 ni wanawake.Mgonjwa wa umri mdogo ana miaka miwili huku wa umri mkubwa akiwa na miaka 98.

Kaunti ya Nairobi imeongoza katika maambukizi mapya kwa kunakili visa 67,Homa Bay na Mombasa visa 11 kila moja, Meru visa Meru 10, Kisumu 8, Kiambu 5, Kilifi 4, Nakuru, Kajiado na Siaya visa 3 kila moja, huku Kakamega na  Machakos zikinali visa 2 kila moja.

Taita Taveta, Garissa, Turkana, Bungoma  na  Narok zimenakili kisa kimoja kila moja.

Wagonjwa 176 wamepona. Hata hivyo wagonjwa wengine wawili wameaga dunia na kuongeza idadi jumla ya vifo kutokana na korona hadi 1,736.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *