NHIF yatakiwa kutoa bima ya matibabu kwa aina zote za magonjwa ya saratani

Muungano wa mashirika ya kukabiliana na ugonjwa wa saratani KENCO unaitaka bima ya kitaifa ya matibabu NHIF kuweka kwa dharura bima maalum kwa aina zote za magonjwa ya saratani.

Kwenye taarifa, KENCO imesema wagonjwa wengi wa Saratani hawana uwezo wa kulipia huduma za magonjwa ya saratani zilizo chini ya mpango uliopo wa NHIF.

Hii inatokana na kwamba wanahitajika kulipa malipo ya bima ya miaka miwili mwanzo ndipo waweze kupata huduma hizo licha ya kadi zao za NHIF kutokuwa na madeni.

KENCO imesema wagonjwa wa saratani hawana uwezo wa kulipa malipo hayo ya juu, hivyo basi hawawezi kupokea huduma hizo muhimu.

KENCO inaitaka NHIF kuandaa kikao cha wadau mbali mbali ili kushughulikia suala hilo.

Na huku dunia inapoadhimisha siku ya ugonjwa wa saratani, KENCO inasema janga la COVID-19 linaendelea kuwaathiri wagonjwa wa saratani.

Limeihimiza serikali irejeshe huduma za kuwapima watu ili kutambua mapema iwapo wanaugua ugonjwa wa saratani, kutoa ufahamu kuuhusu na kuhakikisha kuwepo kwa mazingira bora ya kuutibu.

Muungano huo pia umetoa wito kwa wahudumu wa afya kusitisha mgomo wao ili wagonjwa wa saratani wapokee matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *