Nelson Havi aharamisha maagizo yaliyotolewa kudhibiti mikutano ya hadhara

Rais wa chama cha wanasheria nchini  Nelson Havi amepuuzilia mbali maagizo yaliyotolewa na kamati ya kitaifa ya ushauri wa maswala ya usalama yanayolenga kudhibiti mikutano ya hadhara huku akisema kuwa hayana msingi wowote.

Akiongea huko  Busia alipozuru mahakama ya  Busia, Havi alisema kuwa wakenya wana haki ya kujieleza huku akiongeza kuwa uamuzi huo utahujumu haki na uhuru wa  wananchi.

Havi alisema kuwa katiba hairuhusu kufanywa kwa maamuzi ya kando kando ya barabara huku akiwataka wakenya kujua haki zao za kiraia.

Kuhusu idara ya mahakama, Havi alisema kuwa chama cha wanasheria nchini kinashinikiza matumizi ya teknolojia ili kuimarisha ushirikiano na idara ya mahakama katika kuwawezesha watu wanaozuiliwa korokoroni kupata haki kupitia mifumo ya dijitali.

Alitoa wito kwa wizara ya fedha kusaidia kufanikisha shughuli za idara ya mahakama nchini.

Rais wa chama cha sheria tawi la  Busia  Joseph Makokha alitoa wito kwa idara ya mahakama kushughulikia swala la uhaba wa wafanyikazi katika mahakama ya  Bunyala na kukamilishwa kwa mahakama ya Malaba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *