Ndege za Boeing 737 MAX zarejelea safari nchini Marekani

Ndege za abiria aina ya Boeing 737 MAX zimerejeshwa kwenye huduma nchini Marekani.

Ndege hizo sasa zinafanya safari kati ya majiji ya Miami na New York.

Wasimamizi wa safari za ndege walisitisha huduma za ndege hiyo mwezi Machi mwaka wa 2019 kufuatia ajali mbili mbaya zilizotokea katika kipindi cha miezi mitano.

Halmashauri ya safari za ndege ya Marekani (FAA) iliondoa marufuku hayo mwezi uliopita baada ya makubaliano kuhusu viwango vipya vya usalama wa ndege hizo.

Mruko wa kwanza wa ndege hiyo siku ya Jumanne ulithibitisha usalama wa ndege hiyo aina ya 737 MAX.

Shirika la Ndege la American Airlines lina ndege 31 za abiria muundo huo, ikiwa ni pamoja na saba zilizowasilishwa baada ya FAA kuondoa marufuku hayo mwezi Novemba.

Shirika hilo la ndege na kampuni ya Boeing kwa pamoja zimepanga kuwahakikishia wasafiri kuhusu usalama wa ndege hiyo, japo jambo hilohalitakuwa rahisi kwa mujibu wa kura za maoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *