Ndege ya jeshi ya wanahewa yaanguka Tsavo mashariki

Ndege moja ya kikosi cha jeshi la wanahewa hapa nchini, ilianguka Jumanne asubuhi katika eneo la Irima katika mbuga ya kitaifa ya Tsavo mashariki.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Taita Taveta Patrick Okeri alidhibitisha ajali hiyo na kusema kuwa wataalamu husika tayari wamezingira eneo hilo.

Kulingana na Okeri wachunguzi wa kikosi cha KDF waliwasili kutoka makao makuu ya vikosi vya ulinzi nchini ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Ukurasa rasmi wa facebook wa vikosi vya ulinzi nchini-KDF na ule wa Twitter ulitoa taarifa fupi kuhusiana na ajali hiyo.

Hata hivyo ripoti hiyo haikutaja maafisa waliokuwa katika ndege hiyo.

Habari ambazo hazijadhibitishwa zinadai kuwa kulikuwa na maafisa wanne katika ndege hiyo na hatima yao haijabainika.

Ndege hiyo aina ya Harbin Y-12, ilikuwa imetoka katika uwanja wa  Moi Airbase huko  Eastleigh jijini  Nairobi masaa ya asubuhi ikielekea huko  Voi.

Ajali hiyo ni ya nne kuhusisha ndege za aina hiyo katika muda wa miaka  17 iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *