Categories
Kimataifa

Ndege aina ya Boeing 737 Max kupata idhini ya kupaa bara Ulaya juma lijalo

Mkuu wa shirika la usalama wa ndege barani ulaya EASA,amesema kuwa ndege aina ya Boeing 737 Max zitapata idhini ya mwisho ya kuanza kutumika tena barani ulaya juma lijalo.

Shirika hilo lilisitisha matumizi ya ndege hizo mwezi Machi mwaka 2019, kufuatia ajali mbili za ndege hiyo zilizosababisha vifo vya abiria wengi kutokana na hitilafu za mitambo yake ya kompyuta.

Takriban watu 346 walifariki kwenye ajali hizo mbili katika nchi za Indonesia na Ethiopia.

Ndege hizo ambazo sasa zimefanyiwa marekebisho tayari zimeanza kutumika nchini Amerika na Brazil.

Afisa mkuu wa shirika hilo la EASA Patrick Ky alisema idhini nyingine ya ndege hizo  huenda ikatolewa katika majuma machache yajayo.

Ajali ya kwanza ya ndege hiyo ilitokea mwezi oktoba mwaka  2018 baharini  kwenye pwani ya Indonesia. 

Ajali ya pili ilihusisha ndege aina hiyo ya shirika la Ethiopian Airlines muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji wa  Addis Ababa ikiwa safarini kuja hapa Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *