Categories
Michezo

NAPSA Stars wanoa makali kukabiliana na Gor Mahia Jumapili

Klabu ya NAPSA Stars kutoka Zambia  imeendeleza mazoezi  katika uwanja wa Utalii kujianda kwa mkumbo wa kwanza wa mchujo wa kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirkisho dhidi ya Gor Mahia Jumapili ya Februari 14.

NAPSA inayochezewa na wakenya Shaban Odhonji na beki wa zamani wa Gor David Odhiambo Owino aka Calabar iliwasili nchini Jumatano alasiri.

Gor pia walirejea mazoezini Alhamisi baada ya mgomo wakilalama kutolipwa malimbikizi ya mshahara wa miezi 2.

Mkondo wa pili utasakatwa Lusaka Zambia ,huku mshindi wa jumla akifuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho ambayo Gor wamefuzu mara mbili mtawalia ,mwaka 2018 huku msimu wa mwaka 2018-2019 wakicheza hadi robo fainali.

NAPSA Stars wakiwa maozeizini  uwanja wa Utalii

Gor wanakalia nafasi ya 6  ligini kwa sasa pointi 16 baada ya mechi 9 .

Wageni NAPSA Stars ni klabu iliyobuniwa 1969 lakini ilipandishwa daraja kucheza ligi kuu Zambia mwaka 2012 ikijulikana kama Profund Warriors kabla ya kubadilisha jina ilipotwaliwa na mamlaka ya malipo ya uzeeni  yaani National Pension Scheme Authority Stars huku ikishikilia nafasi ya 13  ligini  kwa alama 18 kutokana na michuano 16 ,alama 10 nyuma ya  viongozi ZANACO.

Mechi ya Jumapili ambayo itakuwa Valentine’s  itaanza saa tisa alasiri katika uwanja wa taifa wa  Nyayo.

Mwamuzi mkuu wa pambano hilo atakuwa Mganda William Oloya na  atasaidiwa na Waganda wenza  Lee Okello atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Isa Masembe msaidizi wa pili   huku  Chelanget Ali Sabila aakiwa afisa wa nne.

Alexis Redamptus Nshimiyimana wa  Rwanda atakuwa kamisaaa wa mechi hiyo  huku Wycliffe Makanga,ambaye ni tabibu wa Harambee Dtars akiwa afisa wa afya kuhusu Covid 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *