Napoli wapoteza pointi 4 kwa kususia mechi ya Serie A

Miamba wa soka nchini Italia Napoli wamepokonywa alama 4 nne kwa kususia mechi ya ligi kuu Serie A ugenini kwa Juventus Oktoba 4 kutokana na wachezaji wake wengi kushikwa na homa ya korona.

Usimamizi wa ligi kuu Italia uliipata Napoli na hatia ya kusisia mchuano Jumatano na kuchukua uamuzi wa kuwaadhibu vikali.

Napoli walidinda kusafiri kuelekea  Turin tarehe 4 mwezi huu baada ya kupata ushauri kutoka kwa maafisa wao wa afya dhidi ya kusafiri baada ya wachezaji wao wawili kupatikana na ugonjwa wa covid 19.

Serie A walikatalia mbali ombi la Napoli kutaka kuahirisha pambano lao dhidi ya Juve na kuwalazimu wasimamizi kuipa  Juventus ushindi wa ubwete.

Kulingana na uamuzi huo Juventus wamepewa ushindi wa mabao 3-0 na pointi 3 huku Napoli wakipokonywa pointi moja ,kuongezea na zile tatu za ushinde.

Matokeo hayo yana maana kuwa Napoli, waliokuwa wameshinda mecghi mbili za kufungua msimu wana pointi 5 huku Juventus wakiwa na pointi 7.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *