Naibu Rais William Ruto awahimiza wakenya kudumisha Amani na Umoja

Naibu wa rais William Ruto ametuma risala ya heri njema kwa waislamu wote wanapoanza mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kwenye ujumbe wake, naibu wa rais alitoa wito wa umoja na mshikamano wakati wa shughuli hiyo ya kimataifa.

Akiongea kwenye video katika mtandao wa Twitter, Ruto aliwahimiza washiriki wote wawaombee wakenya wadumishe amani na umoja katika nyanja zote.

Ramadhan ni mwezi mtukufu wa kufunga, kujichunguza na kusali kwa waumini wa kiislamu.

Inaadhimishwa kuwa mwezi ambao Muhammad alipokea ufunuo wa mwanzo kuhusu Quran ambacho ni kitabu kitakatifu cha waislamu.

Kufunga ni mojawapo wa nguzo tano kuu za Uislamu.

Hii ni mara ya pili waislamu wameadhimisha mwezi wa Ramadhan tangu kuzuka kwa janga la Corona hapa nchini mwezi Machi mwaka uliopita.

Baraza kuu la waislamu hapa nchini-SUPKEM limemtaka rais Uhuru Kenyatta atumie rasilmali za serikali kusaidia jamii ya waislamu hapa nchini wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.

Kaimu mwenyekiti wa kitaifa wa baraza hilo Al Hajj Hassan ole Naado, alisema serikali sekta ya kibinafsi, washirika wa maendeleo wa humu nchini na hata kimataifa wanapaswa kuwasaidia hasa wakati huu ambao ulimwengu unakumbwa na janga la Covid-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *