Nahodha wa Uganda Dennis Onyango astaafu soka kimataifa

Nahodha wa muda mrefu wa timu taifa ya Uganda Dennis Onyango amestaafu soka ya kimataifa.

Onyango ambaye amekuwa kipa chaguo la kwanza wa Uganda Cranes aliandika waraka kwa shirikisho la Uganda FUFA  kustaafu akitaja kuwa aliafikia uamuzi huo mgumu kufuatia ushauri wa familia yake.

“Nimechukua uamuzi huu mgumu baada ya kushauriwa na familia yangu ,nichukue fursa hii kuishukuru familia yangu,meneja wangu na wote waliochangia ufanisi wangu”akasema Onyango

Kwa jumla Onyango ambaye pia anaichezea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, aliichezea Cranes mechi 79  za kimataifa tangu mwaka  2005 dhidi ya Cape Verde.

Kustaafu kwa Onyango aliye na umri wa miaka 35 kunatokea wiki moja baada ya kiungo  Hassan Waswa pia kutangaza kustaafu soka ya kimataifa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *