Mwaniaji urais nchini Uganda ‘Bobi Wine’ aachliwa huru kwa dhamana

Mwaniaji wa urais nchini Uganda Bobi Wine ameachiliwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa kuchangia kusambaa kwa virusi vya corona.

Mahakama iliamua hivyo leo baada ya  Wine mwenye umri wa miaka 38 kuandaa mikutano mikubwa ya hadhara wiki hii.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa mashtaka hayo ya kusambaza virusi vya corona ni kisingizio cha kunyamazisha upinzani nchini humo kabla ya uchaguzi wa tarehe 14 mwezi Januari mwakani.

Ghasia zilizuka na kusababisha vifo vya watu 37 wakati Wine ambaye pia ni mwanamuziki mashuhuri alipokamatwa wiki hii.

Gwiji huyo wa muziki ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, ni miongoni mwa wawaniaji 11 wanaotarajiwa kukabiliana na rais  Yoweri Museveni ambaye amekuwa uongozini tangu mwaka wa 1986.

Makundi ya vijana yaliweka vizuizi katika barabara za mitaa ya  mji mkuu wa taifa hilo  Kampala na mitaa mingine kulalamikia kukamatwa kwa Wine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *