Mwandishi wa Kitabu kinachotahiniwa KCSE aaga dunia

Familia ya Henry Ole Kulet imedhibitisha kifo chake na kuongeza kwamba aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Mediheal huko Nakuru.

Kulet ambaye ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 72, ndiye mwandishi wa riwaya ya “Blossoms of the Savannah” ambayo inatahiniiwa hivu sasa kwa somo la fasihi ya kiingereza kwa mtihani wa kitaifa KCSE nchini Kenya.

Alichapicha kitabu hicho kwa mara ya kwanza mwaka 2008.

Henry alilelewa huko Narok wakati ambapo wakoloni waliagiza kwamba watoto wote wavulana wapelekwe shule na hapo shuleni ndipo alianzia kazi yake ya uandishi akipata motisha kutoka kwa waalimu wake.

Wengi wa wanafunzi hao walihimizwa kujifunza kuhusu ufugaji kwa nia ya kuinua kazi hiyo kwani wengi wa wazazi wao walikuwa wafugaji wa kuhama hama.

Baada ya kumaliza shule ya upili Ole Kulet alijiunga na taasisi ya Egerton ambapo pia alipata kujifunza kazi ya kusimamia mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na wazungu.

Baadaye Henry aliajiriwa kama msimamizi msaidizi wa shamba na “Kenya Farmers Association” na akachapisha kitabu cha kwanza kiitwacho, “Is it possible”.

Alistaafu kama msimamizi wa shamba mwaka 1987 akiwa na umri wa miaka 41 ili kuangazia kikamilifu uandishi wa vitabu na amekuwa na taaluma ya kufana kama mwandishi kwa miaka 33 sasa.

Vitabu vingine ambavyo Henry Ole Kulet aliandika ni kama vile, “Bandits of Kibi”, “Daughter of Maa” na “How to become a man”. Ole Kulet aliwahi kushinda tuzo la fasihi la Jomo Kenyatta ambalo ndilo tuzo la fahari zaidi nchini Kenya kwa waandishi wa fasihi mara tatu.

Mwaka 2019, Rais alimtuza medali ya “Elder of the Burning Spear” kutokana na mchango wake kwenye fasihi ya nchi hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *