Mwanawe Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri afariki kutokana na COVID-19

Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amepoteza mwanawe Arthur Kinyanjui aliyeaga dunia Jumatatu kutokana na maradhi ya COVID-19.

Kinyanjui amefariki alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Aga Khan Mombasa alipokuwa amelazwa tangu mwaka uliopita akiwa na nimonia na matatizo ya kupumua.

Kwa masikitiko, Ngunjiri amemwomboleza mwanawe Arthur, ambaye ndiye kitinda mimba, na kumtaja kuwa mwenye bidii.

Naibu Rais William Ruto ametuma rambi rambi kwa familia hiyo na kumuelezea Kinyanjui kuwa mwenye busara na mtu wa bidii, aliyefanikiwa katika biashara na ukulima.

“Tunaomba Mungu kwamba familia ya Ngunjiri, marafiki na wakazi wa Eneo Bunge la Bahati wapate nguvu na faraja wakati huu mgumu,” akasema Ruto.

Naye Mbunge wa Gilgil Martha Wangari pia amesema, “Faraja zangu za dhati kwa rafiki yangu Kimani Ngunjiri kwa kumpoteza mwanawe Arthur Kinyanjui almaarufu AK47.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *