Mwanaume ampokonya polisi bastola na kuwaua watu wawili Kisumu

Mwanamume mmoja wa umri wa makamo Ijumaa asubuhi alimpokonya bastola afisa wa polisi, na kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wawili katika kituo cha mabasi cha Kisumu, na kuwajeruhi wengine kadhaa.Kulingana na polisi,bastola hiyo ya aina Ceska ilikuwa na risasi 14.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Kisumu Samuel Anampiu amesema watu hao wawili waliopigwa risasi kifuani walifariki wakipelekwa hospitali ya rufa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga.

Watu wengine wanne pia wamelazwa katika hospitali hiyo,mmoja wa akiwa katika hali mahututi.

Komanda huyo polisi amesema mwanamume huyo alikuwa na watu wengine wawili alipomshambulia polisi huyo, aliyekuwa akiyaelekeza magari katika mzunguko wa barabara wa Kisumu Boys.

Wakazi waliokuwa na ghadhabu walimuua mwanamume huyo kwa kumpiga kwa mawe.

Anampiu amesema polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo na kutoa wito kwa wakazi kutoa kwa polisi habari zitakazowawezesha kuwatia nguvuni washukiwa wengine wawili ambao wametoroka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *