Categories
Burudani

Mwanamuziki wa Marekani Offset akamatwa na polisi

Mwanamuziki wa mtindo wa kufokafoka nchini Marekani kwa jina Offset alikamatwa na polisi katika eneo la Beverly Hills jumamosi jioni saa za Marekani.

Offset ambaye jina lake halisi ni Kiari Kendrell Cephus alikuwa akiendesha gari ambamo walikuwa na binamu ya mke wake Cardi B, ambaye anafahamika kama Marcelo Almanzar.

Offset alikuwa mbashara kwenye akaunti yake ya Instagram wakati akitiwa mbaroni ambapo kwanza anakataa wito wa polisi wa kujisalimisha na baadaye polisi hao wanamtoa kwenye gari lake kwa nguvu.

Kwenye video hiyo Offset anaelezea kwamba watu ambao walikuwa kwenye kampeni, kupigia debe mwaniaji urais wa Marekani wa chama cha Republican ambaye pia ni rais wa sasa wa Marekani Donald Trump, waligonga gari lake mara kadhaa na bendera ya nchi ya Marekani.

Maafisa wa polisi nao wanaelezea kwamba walipata ripoti kwamba abiria kwenye gari la Offset alilenga mtu aliyekuwa akitembea kwa miguu na bunduki.

Baada ya majadiliano Offset aliachiliwa huru ila Marcelo wa miaka ishirini anasemekana kukamatwa hadi sasa kwa kosa la kuwa na silaha iliyofichwa na kuwa na bunduki ambayo ina risasi katika eneo la umma.

Dhamana ya binamu huyo wa Cardi B inasemekana kuwa dola elfu 35 sawa na milioni 3.8 pesa za Kenya. Cardi B aliandikisha nia ya kutaka kutalikiana na Offset mwezi Septemba mwaka huu lakini baada ya mume wake kumpa zawadi siku yake ya kuzaliwa, wawili hao walirudiana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *