Categories
Habari

Mwanamume auawa na ndovu Mtito Andei

Mwanamume mwenye umri wa miaka 73 amefariki papo hapo baada ya kukanyagwa na ndovu katika eneo la Nthunguni katika Kata ya Mtito Andei, Kaunti Ndogo ya Kibwezi Mashariki.

Muathiriwa huyo aliyetambuliwa kama Charles Mutinda Mutisya ameuawa na ndovu huyo alipokuwa akielekea shambani kwake kulima.

Ndovu huyo alikuwa ametoka katika Mbuga ya Kitaifa ya wanyama pori ya Tsavo Mashariki.

Akiongea na Shirika la Habari nchini, KBC, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Makueni Joseph Ole Naipeyan amethibitisha kisa hicho.

Naipeyan amesema maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Mtito Andei na Shirika la Huduma kwa wanyama pori (KWS) wamezuru eneo la kisa hicho na kupata mwili wa muathiriwa ukiwa na majeraha.

Mwili huo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Makindu kufanyiwa uchunguzi wa upasuaji wa maiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *