Mwanamke ashtakiwa Kilifi kwa madai ya wizi wa mtungi wa gesi

Mwanamke mmoja amefikishwa mahakamani baada ya kudaiwa kuiba mtungi wa gesi kutoka kwa nyumba ya jirani yake katika eneo la Mtaani, Mjini Kilifi.

Stella Mosy, mwenye umri wa miaka 32, anadaiwa kuwa mnamo tarehe 23 mwezi huu, aliingia nyumbani mwa Calvin Omondi na kutoweka na mtungi wa gesi wa kupikia.

Mahakama imeelezwa kwamba mlalamishi alikuwa ametoka kidogo nyumbani mwake lakini kabla kufika mbali, akamuona mwanamke huyo akitoroka na mtungi huo.

“Nilikuwa nimefika umbali wa kama mita 20 nilipomuona anatoroka na mtungi wangu wa gesi, nikapiga nduru, watu wakaja kunisaidia tukamkamata na kumpeleka hadi kituo cha polisi,” akaeleza Omondi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Sifuna Daniel Sitati, mshukiwa huyo amekanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50 au shilingi elfu 10 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 17 Februari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *