Mwanamke anayedaiwa kuiba kompyuta ya Spika Pelosi Marekani atiwa nguvuni

Mfuasi mmoja wa Donald Trump anayeshukiwa kuiba kipakatalishi kutoka kwa afisi ya Spika Nancy Pelosi wakati wa uvamzi wa jengo la bunge nchini Marekani amekamatwa.

Riley June Williams, mwenye umri wa miaka 22, alikamatwa huko Pennsylvania kwa mashtaka ya kuzua vurugu na kuingia kinyume cha sheria katika jengo la bunge.

Mpenziwe wa zamani alisema kupitia hati ya kiapo kwamba Williams alikusudia kuuza data iliyokuwa kwenye kipakatalishi hicho kwa majususi wa Urusi.

Watu watano walifariki baada ya kundi la wafuasi wa Trump kuvamia jengo la Bunge tarehe sita mwezi huu.

Kesi ya Williams ni moja tu kati ya zaidi ya kesi 200 ambazo zimefunguliwa tangu uvamnizi huo uliotekelezwa wakati wabunge walipokutana kuthibitisha uchaguzi wa Joe Biden.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *