Categories
Habari

Mvua kubwa inatarajiwa siku ya Ijumaa hapa nchini

Idara ya utabiri wa hewa nchini imeonya kwamba mvua kubwa inatarajiwa siku ya Ijumaa katika maeneo ya magharibi,mlima Kenya,kusini mashariki pamoja na kaskazini mashariki mwa nchi.

Idara hiyo kwenye taarifa ilisema mvua hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Jumamosi katika sehemu za nyanda za juu magharibi mwa Rift valley pamoja na nyanda za juu mashariki mwa Riftvalley.

Idara hiyo iliongeza kwamba mvua hiyo huenda ikapungua siku ya jumapili.

Idara hiyo imewashauri wakazi  kujihadhari na mafuriko ya ghafla katika maeneo ambayo huenda yasipokee mvua.

Aidha idara hiyo imeonya dhidi ya kuendesha magari au kutembea kwa maji ambayo yanasonga kwa kasi au katika sehemu zilizowazi.

Wananchi pia wameonywa dhidi ya kujikinga mvua chini ya miti na pia kujiepusha na radi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *