Muuaji sugu awahofisha wakazi wa Moi’s bridge

Wakazi wa mji wa Moi’s Bridge katika kaunti ya Uasin Gishu wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na muuaji sugu katika sehemu hiyo.

Hii inafuatia kisa cha Ijumaa usiku ambapo mlinzi mmoja wa usiku aliuawa na mwili wake kukatwakatwa.

Mlinzi huyo David Mwiti wa umri wa miaka 30 alikuwa akilinda jengo moja la kibiashara na wakazi walipata ameuawa Jumamosi asubuhi.

Wakazi wanawalaumu maafisa wa polisi wa utepetevu na kutaka wahamishwe kwa sababu wamehudumu kwa muda mrefu katika kituo kimoja cha polisi.

Wakazi pia wanataka makachero wa DCI wachunguze kwa kina msururu wa mauaji katika sehemu hiyo.

Mlinzi huyo ameuawa wiki mbili baada ya mlinzi mwingine kuuawa na watu wasiojulikana.

OCPD wa Moi’s Bridge Fanuel Nasio amesema uchunguzi wa mauaji hayo umeanzishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *