Kocha wa Harambee Stars Jacob Ghost Mulee ametaja kikosi cha wachezaji 28 wanaopiga soka humu nchini kujiandaa kwa mechi mbili za mwisho za kundi G mwezi ujao kufuzu kwa mashindano ya kombe la AFCON mwaka ujao nchini Cameroon.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa kikosini kwa mara ya kwanza ni kipa wa KCB Joseph Okoth na mchezaji mwenza Nahashon Alembi pamoja na kiungo wa AFC Leopards Collins Shichenje huku pia kiungo wa Wazito FC kevin Kimani akijumuishwa kikosini kwa mara ya kwanza.
Henry Mejja ambaye ni mshambulizi kutoka Tukser Fc aliyefanya vyema katika mashindnao ya CECAFA kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 mwaka jana pia amejumuishwa kikosini huku wakitarajiwa kuripoti kwa mazoezi ya kambi Jumatatu ijayo.
Kikosi kilichotajwa kinawajumuisha:-
Makipa
Brian Bwire (Kariobangi Sharks), James Saruni (Ulinzi Stars), Joseph Okoth (KCB), Peter Odhiambo (Wazito)
Mabeki
Johnstone Omurwa (Wazito), Michael Kibwage (Sofapaka), Samuel Olwande (Kariobangi Sharks), Nahashon Alambi (KCB), Bonface Onyango (Kariobangi Sharks), David Owino (KCB), Daniel Sakari (Kariobangi Sharks), Baraka Badi (KCB)
Viungo
Lawrence Juma (Sofapaka), Kenneth Muguna (Gor Mahia), Collins Shichenje (AFC Leopards), Micheal Mutinda (KCB), Musa Masika (Wazito), John Macharia (Gor Mahia), Reagan Otieno (KCB), James Mazembe (Kariobangi Sharks), Oliver Maloba (Nairobi City Stars), Bonface Muchiri (Tusker), Kevin Kimani (Wazito), Abdalla Hassan (Bandari)
Washambulizi
Erick Kapaito (Kariobangi Sharks), Elvis Rupia (AFC Leopards), Henry Meja (Tusker), Benson Omalla (Gor Mahia)
Stars iliyo ya tatu kundi G kwa pointi 3 baada ya mechi 4 itawaalika Misri tarehe 22 mwezi ujao kabla ya kuhitimisha ratiba ugenini tarehe 30 mjini Lome Togo.
Misri na Comoros wanaongoza kundi hilo kwa alama 8 kila moja wakisaka alama 1 kutoka kwa mechi mbili zilizosalia ili kufuzu kwenda AFCON mwakani.