Mudavadi: Ni muhimu kutambua kasoro zilizochipuza wakati wa vita dhidi ya Covid-19

Serikali imetakiwa kuchunguza kwa makini na kufafanua kasoro zilizoshuhudiwa wakati wa vita dhidi ya virusi vya corona.

Akiongea wakati wa kongamano la kitaifa la kutathmini hali ya janga la COVID-19 hapa nchini, Kiongozi wa chama cha Amani National Congress  Musalia Mudavadi alisema licha ya kuwa juhudi kabambe zimefanywa ili kukabiliana na janga hilo, kuna haja ya kuchunguza juhudi hizo zote kwa mtazamo maalum.

Alisema kuwa kunapaswa kuwa na mjadala wa umma kuhusu nani amekuwa katika mstari wa mbele  kukiuka masharti ambayo yaliwekwa kudhibiti virusi hivyo vya Covid-19.

Mudavadi alisema kuna haja kubwa ya kuchunguza sera ya ustawi wa kitaifa kuhusiana na majukumu ya serikali ya taifa na serikali za kaunti.

Alitoa wito kwa serikali kuchunguza upya mfumo wa kutoza ushuru ili kuhakikisha kuwa unakubalika zaidi kwa jamii ya wafanyibiashara.

Kulingana na Mudavadi, taasisi nyingi zimeathirika vibaya na shinikizo kuongezeka kwa biashara ndogo ndogo kutokana na janga la Corona.

Matamshi ya Mudavadi yanawadia siku moja baada chama cha Madaktari kuelezea wasiwasi kuhusu mikusanyiko ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *