Categories
Kimataifa

Muda wa kuapishwa kwa mawakala wa uchaguzi kufungwa Oktoba 23

Shughuli ya  kuapishwa kwa mawakala wa vyama vya siasa katika  uchaguzi mkuu nchini Tanzania kukamilika Ijumaa hii  huku uchaguzi mkuu  ukiandaliwa  tarehe 28 Oktoba, 2020.

Zoezi hilo liliongezewa muda kutoka tarehe 21 hadi 23 Oktoba kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Dkt Wilson Mahera Charles .

Dkt .Mahera  alisema waliafikia uamuzi huo kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na changamoto ya kutofikika kwa urahisi kutokana na jiografia na hivyo kuwa vigumu kwa wasimamizi wa uchaguzi kuwafikia na kuwaapisha mawakala hao kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Dkt  Mahera  alivitaka vyama vya siasa vipeleke orodha ya mawakala wao na viwe vimewapanga mawakala hao katika vituo vya kupigia kura na kuweka namba ya simu ya kila wakala husika.

Dkt  Mahera amevitaka vyama  vya siasa kufuata utaratibu wa kisheria na kwa mujibu wa maelekezo kwa vyama vya siasa na wagombea vitapata fursa kwa mawakala wao kuapishwa.

Mawakala wa vyama 19 vya siasa vilivyosajiliwa  wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na Urais.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *