Mtetezi wa haki za binadamu Edwin Kiama aachiliwa bila masharti

Mahakama ya Milimani imemwachilia huru mtetezi wa haki za binadamu Edwin Kiama bila masharti baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha ushahidi dhidi yake.

Hakimu mkuu Jane Kamau pia aliagiza Kiama arejeshewe shilingi laki tano alizokuwa amelipa kama dhamana.

Akitoa uamuzi huo, hakimu mkuu Jane Kamau alisema vifaa vilivyotwaliwa kutoka kwa Kiama ikiwemo rununu na vipakatalishi viliwasilishwa kwa halmashauri ya mawasiliano na ripoti ya uchunguzi wa vifaa hivyo haijatolewa.

Kiama alikamatwa kwa madai ya kuchapisha taarifa za kushinikiza shirika la fedha duniani-IMF, kukomesha utoaji mikopo kwa Kenya.

kesi hiyo itatajwa tarehe 21 mwezi Mei mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *