Msiwafukuze wanafunzi kwa sababu ya karo, aonya Prof Magoha

Waziri wa elimu Profesa George Magoha amewatahadharisha wasimamizi wa shule dhidi ya kuwafukuza wanafunzi shuleni kuhusiana na malimbikizi ya karo.

Kulingana na Prof Magoha njia bora ni kutafuta kushauriana na wazazi  ama walezi jinsi ya kulipa karo.

Profesa Magoha alisema serikali haitavumilia matendo kama hayo kutoka kwa wasimamizi wa shule ambao alikariri kwa sasa hawana mamlaka ya kuwafukuza wanafunzi.

Magoha alikuwa akiwahutubia wana-habari kwenye shule ya msingi ya Kosawo iliyoko eneo la Manyatta ambako alikadiria uwasilishwaji wa madawati shuleni.

Magoha alisema shule nyingi za sekondari za mabweni  zilikuwa zimehifadhi chakula kingi kilichofaa kutumiwa na wanafunzi wakati wa likizo ndefu  na hivyo hazina sababu za kuwafukuza wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *