Msimu mpya wa ligi kuu Italia Serie A kung’o a nanga kesho

Msimu mpya wa ligi kuu nchini Italia Serie A  mwaka 2020/2021 utaanza rasmi kesho baada ya mapumziko mafupi.

Sawa na ligi nyinginezo barani ulaya,ligi ya Serie A pia imechelewa kuanza kutokana na janga la covid 19 lililochelwesha kumalizika kwa msimu wa mwaka 2019/2020.

Timu za Benevento,Crotone na Spezia zimepandishwa ngazi kushiriki ligi hiyo msimu huu huku pia mabingwa wattezi Juventus wakianza maisha mapya chini ya ukufunzi wa kiungo wa zamani Andrea Pirlo.

Hati uteuzi wake Pirlo amekuwa kocha wa timu ya Juventus ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23 .

Pirlo aliipigia Juve mechi 119 baina ya mwaka 2011 na 2015 na kufunga mabao 16.

Katika mechi za ufunguzi wikendi hii,Kesho  Fiorentina wako nyumbani dhidi ya Torino nao Hellas Verona iwatumbuize As Roma.

Jumapili mikwangurano minne itapigwa Napoli wakiwa ziarani kwa Parma,Genoa imenyane na Crotone wakati Sassuolo ikichuana na Cagliari nao Juventus wakabane koo na Sampdoria .

Ac Milan wataanza kazi jumatatu usiku ugani San siro dhidi ya Bologna.

Ligi hiyo itakamilika Mei 23 mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *